Sababu 10 Za Wewe Kuwa Mpweke/Single Na Kukumbwa Na Misukosuko Ya Mahusiano


Wakati ambapo unadeti mwanaume kuna ile tabia ya ghafla inayokuja ambayo unajaribu kumkosoa kila kitu ambacho unakiona si sawa kwake ili uweze kuendelea na shani yako ya kumtafuta mwanaume alie sawa aka Mr. Right. Lakini iwapo utakuwa ukiendelea kumtafuta mr Right zaidi na zaidi labda kutaashiria ya kuwa kumpata huyo mr Right si shida ya kwako. Labda wewe ndiwe shida ya kuwa single hadi sasa.


Wakati ambapo wanawake hukua, hupenda sana kujikita kuangalia filamu, tamthilia za mahaba ambazo zinajenga dhana ya kuwa mr Right anaweza kutokea siku moja katika maisha ya mwanamke. Dhana hii imekuwa ikiendeshwa na movie nyingi kama vile za Cinderella nk ambapo mhusika anapendwa na mwanaume aliyekutana naye kighalfa na mwishowe wanaishi maisha ya raha mstarehe.
Well, hizo ni ndoto ambazo haziwezi kutimia na unafaa kuamka kutoka katika ndoto uliokuwa ukilala na kuikumbatia ulimwengu wa uhalisia.

So, sababu za wewe kuwa single mpaka sahizi ni zipi?

Kiukweli ni kuwa hakuna mtu anaishi maisha ya cinema. Kama umekuwa ukitafuta kuwa na uhusiano lakini unashindwa kuwa na mafanikio, unahitaji kusoma baadhi ya sababu ambazo tumeziorodhesha.

1. Una orodha ulioiandika
Wanawake wote huwa na mawazo ya mr Right kwa akili zao.  Kawaida huwa ni yule ambaye anapatikana katika filamu na sinema. Iwapo una orodha ambayo umeiandika, orodha hio inafaa iwe kama mwongozo tu.

Kama uko mbioni kutafuta mahusiano na mwanaume mwenye kima cha futi sita, mhandsome, mwenye uwezo kifedha, macho ya hudhurungi,  mjanja, mzuri, unafaa kufahamu ya kuwa mwanaume huyo anaweza kupatikana ila tu anaweza kuwa si mwenye kima cha futi 6 ama mwenye macho ya hudhurungi. Kama atapata wa futi 5 na nchi 9 kumbuka kuwa orodha yako haufai kuitilia maanani sana. 

Kiufupi ni kuwa haufai kuizingatia orodha yako ulioiandika asilimia 100, si lazima upate mwanaume ambaye ana masharti yote ambayo unataka.

2. Unatext wanaume wengi kupita kiasi
Ni hisia iliyo ya juu kujua kuwa unapendwa, unababaikiwa na kuhangaikiwa. Lakini kama utaanza kuongea na mwanaume, ukaenda naye deti mara kadhaa, na kuanza kudhania ya kuwa ni boyfriend wako, basi unafaa kuwapotezea wale wengine na uache kuongea nao asilani.

Kama hauwezi kujizuia kuzungumza na mtu mmoja, na kila wakati ambapo utakuwa ukileta gumzo la kuwa huwezi kuacha kuchat na wanaume wengine fahamu ya kuwa unamsukuma mbali mwanaume ambaye umemzimia.
Haya ni mambo mawili ambayo anaweza kuamua kuchukua: anaweza kukuambia uachane na kutext hao wanaume wengine ama atachoshwa na kuskia gumzo lako la kila wakati ambalo unawataja wanaume wengine mara kwa mara. Hivyo kama unachat na wanaume wengine wengi, jua ya kuwa yule ambaye uko naye kwa sasa anaweza kuona ya kuwa hauko interested na yeye.

3. Unaongea ubaya kuhusu marafiki zako
Kuongea ubaya kuwahusu marafiki zako kwa mwanaume umemzimia ni jambo ambalo unafaa kuacha. Hakuna mtu ambaye angependa kuhusishwa na mwanamke mlalamishi ama malkia wa drama, na iwapo unaongea mabaya kuhusu marafiki zako huwa unaongea nini kingine?

Baada ya muda ataanza kuingiwa na maswali ya mbona bado uko na marafiki zako, na pia anaweza kuingiwa na mawazo ya kuwa pindi mtakapokuwa katika mahusiano utakuwa ungeongea uchafu na ubaya kumhusu na marafiki zako.
Hakuna mwanaume ambaye yuko radhi kuwa na mahusiano na mwanamke ambaye ana uhakika wa kuwa ataanza kutoboa siri zake kwa marafiki zake.

4. Unachezewa, na kila mwanaume anachukiza
Ni kweli kuwa kila mtu ashawahi kuwa na mahusiano mabaya na mwanaume mara moja au nyingine. Ashawahi kufikia hatua ya kuwachukia wanaume kiasi cha kuwa hautamani kuongea nao kabisa. Kama wewe ni mwanamke ambaye ushawahi kuwa katika mahusiano ambayo ulichezewa, na umeshindwa kuvumilia na kuyasongeza maisha yako, inakubalika. Mambo kama haya huchukua muda hadi yatakapoisha.

Lakini kama uko katika deti na mwanaume, haufai kuongea wakati wote kuhusu ubaya wa ex wako na jinsi ambavyo alivyokuumiza, jinsi unavyofikiria kuwa wanaume wote ni waongo na wadanganyifu, na jinsi ambavyo hutambui iwapo mapenzi ya kweli yanaweza kupatikana dunia hii. Mwanaume unayetoka naye deti si chanzo cha kwako kukosana na ex wako hivyo hupaswi kumlalamikia bali unafaa kukubali matokeo yaliyofanyika awali na kusongea mbele na maisha yako. Kama unaogopa na swala la kuwa unaweza kudanganywa, basi tatua shida zako ukiwa single.

5. Hautaki kufanya kazi
Kama ndoto yako ni kuwa unatamani kuwa mama wa nyumbani, ni vizuri. Lakini katika deti ya kwanza na mwanaume hana haja ya kusikia mambo kama hayo. Wanataka kukutana na wewe, lakini kuona sehemu yako ambayo uko mchangamfu. Wanataka kuona sehemu yako ya shangwe, ki wewe ambaye una furaha na mtu wa ashki.

Wanaume hawapendi kujihisi kama unawaangalia wao, kupanga harusi, watoto wangapi utapata, na chochote kile ambacho kitakuwa kikizulika kwa akili yako. Kila mtu ana mawazo ya fumba kwa akili yake, hivyo yanafaa kubaki akilini mwako na si kila mtu anahitaji kujua. Wanaume hawapendi presha, haswa ile ambayo inajitokeza katika deti ya kwanza. Wanaweza kujua dalili iwapo mwanamke anataka kuolewa kama kesho! Hivyo acha tabia za tai.

6. Unapinga kila wakati
Kama unaongea na mwanaume halafu akakuuliza ufanye kitu flani, lakini kila wakati unapinga, itafika wakati flani ataacha kukuuliza. Kama tu vile ukiwa na marafiki zako, nadhani ushawahi kukumbwa na kutohusishwa na jambo fulani, halafu baadae marafiki zako wakakuambia kuwa imetokana na kuwa unakataa vitu ambavyo unaagizwa kufanya.  Iwapo kila wakati unakuwa mgonjwa, unafanya kazi, unafanya kitu fulani, basi pia utakuwa single milele.

7. Mitandao ya kijamii umeifanya maisha yako
Ok mitandao ya kijamii ni mizuri kutangamana na wenzako, lakini usiifanye kama ni sehemu ya kwako kunyatia profile za wengine, haswa kwa mwanaume ambaye unadeti naye. Ukianza kudeti na mwanaume, utakuwa ukiyaingia maisha yake, na hii itakufanya mtu mgeni kwa maisha yake.

Ok ni hivi, hufai kuichunguza akaunti yake kabisa sababu unaweza kuona comments, picha nk ambazo zinaweza kukuchanganya. Usijishughulishe kuangalia vitu ambavyo hujahusishwa. Hii ni kwa sababu unaweza kuona comment ama picha iliyotumwa kwakwe na mwanamke flani, jambo ambalo hutalichukulia vizuri.

8. Kushtushwa na mwanaume ambaye anaonyesha maridhia kwako
Hii ni muhimu sanaa. Kama wewe ni yule ambaye anashtushwa ama kushangazwa na jinsi mwanaume anaonyesha uzuri na upendo kwako, kama vile kukusifu, kukufungulia mlango, kulipia gharama zako, ama kimsingi kukutumikia vile unavyotaka wewe, basi bila shaka wewe ndiwe tatizo lako mwenyewe.

Relax na utulie, usichukulie kana kwamba yeye anakufanyia hivyo akiwa na ajenda zake fiche. Kama utaonyesha dalili za kutomwamini basi utamfanya ahisi ya kuwa huthamini kile ambacho anajaribu kukuonyesha ama kukufanyia.

9. Kuwa na mtihaji mwingi
Uhitaji ni ile tabia ambayo unajipendekeza kwake mara nyingi. Mwanamke hafai kuwa masaa 24/7 anataka kuwa kando na mwanaume. Unafaa mara moja au nyingine kuwa na shughli zako mwenyewe. Ukiwa kila wakati utakuwa na mwanaume basi anaweza kukuzoea na kukudhalilisha ama kuchukizwa nawe. 
Mahusiano yanahitaji muda mpaka yakolee, si eti utapata mpenzi wako chini ya masaa 48. Mwanzo unafaa umpe nafasi ya yeye kujiskia huru kwa kumpa nafasi kutangamana na marafiki zake na wewe kuenda kujumuika na wanawake wenzako.

10. Unapenda kuwa na marafiki zako wa dhati kila wakati
Kama wewe ni yule ambaye kila wakati anakuwa na rafiki yake ukitaka usaidizi wa kimawazo, maoni, mtizamo wake ikija na maswali ya maisha yako yakudeti, inamaanisha ya kuwa huna usalama kujihusu wewe mwenyewe na huna uwezo wa kujiamulia.

Ni vizuri kujumuika na marafiki zako lakini haina haja ya kuwajuza kuhusu chochote ambacho kinahusiana na maongezi, matatizo ama chochote kuhusu boyfriend wako. Kuna vitu vingine havina haja kuvieleza hadharani kwa marafiki zako.



No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.