Unampenda mpenzi wako lakini unaona ya kwamba anakupuuza. Hali kama hii itahitaji ubadilishe tabia hio ili uweze kuwa na maisha mazuri na mpenzi wako.
Kuteka atenshen kwa mpenzi wako ni rahisi kama mara kwa mara mnakua pamoja. Lakini kuna mambo ambayo lazima pia yazingatiwe ili kupuuza huku kwa mpenzi wako kupotee kabisa.
Hivyo kando na kuwa mnakutana mara kwa mara chuoni, kazini, mtaani ama sehemu yoyote ile lazima uwe na uhakika wa kuwa kuna mambo unayopaswa kufanya ili kumfanya mpenzi wako asikupuuze tena.
Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia ili uweze kuteka atenshen ya mpenzi wako.
#1 Mahusiano yenu ni gani?
Kabla kusonga mbele lazima utambue wewe na mpenzi wako mko katika mahusiano yapi. Mara nyingi watu wengi huchanganya kati ya mahusiano, mapenzi na urafiki. So hapa lazima ujue mahusiano yenu hapa yana lengo gani maana unaweza kuwa unadhania uliye naye ni mpenzi wako kumbe ni rafiki tu. [Soma: Jinsi ya kuuhepa mtego wa kuwa rafiki ya mwanamke unayempenda]
#2 Ni hatua gani anazozipitia katika maisha yake muda huo?
Wakati mwingine mpenzi wako anaweza kukupuuza bila kukuambia sababu yeyote. Hivyo lazima umchunguze kwanza. Unaweza kupata anasumbuliwa na msongo wa mawazo, labda ni fikra za mitihani, kazini ama chochote kile. Hivyo inakupasa uzingatie yale mambo ambayo yanamsumbua mpenzi wako wakati huo kabla ya kuchukua wazo la kuwa anakupuuza.
#3 Mjulie hali.
Mpenzi wako anaweza kuwa anakupuuza, lakini lazima utambue ya kuwa utalazimika umjulie hali umuulize lile ambalo linamsumbua. Hapa unafaa umuulize iwapo anahitaji muda wa zaidi kuspend time na yeye ama ni kitu gani ambacho anahitaji kutoka kwako.
#4 Mawasiliano.
Ikija katika maswala ya kupata atenshen kutoka kwa mpenzi wako, lazima uwe mstari wa mbele katika mawasiliano. Hakikisha ya kuwa wewe na mpenzi wako mnakuwa na muda wa kuongea zaidi. Hii ni njia moja wapo nzuri ya kuiteka atenshen ya mpenzi wako. [Soma: Formula za kumtumia mwanamke SMS ili aweze kureply fasta]
#5 Kuwa na lengo.
Kama mmekubaliana ya kuwa mtakuwa mnaspend time mkiwa pamoja, basi itakubidi upange siku na wakati ambapo mtakuwa mnakutana kila wiki. Hii ni njia moja wapo nzuri ya kutumia kuiteka atenshen ya mpenzi wako.
#6 Kuwa mfaano mwema kwake.
Kama unataka mpenzi wako awe mstari wa mbele kukusaprise na mambo kadhaa, basi unapaswa kuanza wa kwanza kumfanyia mambo kama hayo. Huu ndio unaitwa mfano mwema na ambao mpenzi wako anaweza kuuiga kirahisi.
#7 Usifiche hisia zako.
Ukitaka atenshen ya rahisi kutoka kwa mpenzi wako, haupaswi kuficha hisia zako. Kama una kitu ambacho kinakusumbua basi unafaa umweleze mpenzi wako bila kuficha. Hii ni nguzo muhimu katika kumfanya mpenzi wako kukupenda zaidi na kukupa atenshen nyakati zote.
Upo! [Soma: Jinsi ya kutambua kama mpenzi wako amekamilika]
No comments:
Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA