Mambo 9 Muhimu Ya Kufanya Ukiwa Mjamzito


Baada ya kugundua kuwa umekuwa mjamzito, kuna mambo muhimu ambayo unapaswa kufanya na kuzingatia ili uwe na afya njema kwako na pia kwa mtoto unayetarajia. Kujua iwapo wewe ni mja mzito au la ni muhimu kwa kuwa kutakusaidia kupanga mikakati ambayo itakufanya wewe na mwanao mtarajiwa kuwa na siha bora pindi unapojifungua. [Soma: Jinsi ya kutambua kama una ujauzito]


Unapokuwa mjamzito, kawaida utakumbana na mambo na itikadi nyingi ambazo zinaambatanishwa na uja uzito. Mambo hayo kawaida mengine huweza kuwa ya kweli ilhali mengine ni ya kuyaskiza tu.

Leo Nesi Mapenzi tumekuja na mambo ambayo unafaa kuzingatia ukiwa umeshika mimba. Zama nasi.


1. Anza kwa kumeza tembe za vitamini

Inashauriwa ya kuwa mwanamke anapaswa kumeza tembe za vitamini kabla ya kupata ujauzito, lakini kwa kuwa umejua sahizi, ni bora uanza kumeza dawa hizi kwa sasa. Vitamini hizi ni kama vile folic acid, iron na calcium. Hii huhakikisha ya kuwa mtoto anakuwa na virutubishi vinavyofaa ili kukua kunakostahili.

2. Kula chakula cha afya

Kando na kuwa mtoto atahitaji vitamini, kuna madini mengine ambayo hupatikana ndani ya chakula kama vile carbohydrate na proteins. Hizi zinapatikana kwa kula vyakula kama vile mkate, mchele, mahindi, samaki, maharagwe, nyama, mayai na kadhalika. Pia ulaji wa mboga na matunda husaidia pakubwa kukupatia madini haya.

3. Fanya mazoezi

Ujauzito unataka mtu ambaye ni mchangamfu. Kufanya mazoezi mara kwa mara humsaidia mwanamke mjamzito kuwa na nguvu na afya. Hii inaweza kutimizwa kupitia kutembea, kukimbia na pia kuenua vitu vizito.

4. Jipatie usingizi

Usingizi ni muhimu kwa mjamzito. Usingizi huwa na manufaa kwako na kwa mtoto wako. Kama unapata matatizo ya usingizi itabidi ujitaftie wakati mwafaka ambao unaona ni rahisi kwako kupata usingizi kwa haraka.

5. Pata chanjo

Chanjo ni muhimu kwa kuwa humsaidia mtoto wako kujikinga kutokana na athari za magonjwa mabaya. Hivyo ni lazima uwe unapata chanjo mara kwa mara kulingana na ushauri uliotoka kwa daktari.

6. Tembea hospitali upate huduma za kliniki

Ni muhimu kwa mjamzito kutembelea kituo cha afya ili kuangaliwa afya yake na mtoto. Hii nikuanzia kupimwa kiwango cha damu, uzani, kupewa dawa na pia kuangalia jinsi mtoto anavyoendelea.

7. Epuka misongo ya mawazo (stress)

Hakikisha unaepuka stress kwa kuwa ni kichocheo ambacho hufanya mtu kupoteza  hamu ya kula, huongeza presha, huumiza kichwa na hali nyingine nyingi.

8. Jielimishe kuhusiana na ujauzito

Ujauzito una mambo mengi hivyo unapaswa kujielimisha na kujifunza mambo yote ambayo yanahusiana kuhusu ujazito. Hii itakupa nafasi ya kuelewa mambo yote ambayo utapitia kuanzia kupata ujauzito, kujifungua na pia mambo ya kufanya utakapojifungua.

9. Usilewe, usivute, wala usitumie mihadarati

Kufanya moja wapo ya mambo haya kunaathiri ukuaji wa mtoto. Matumizi haya huweza kumuumbua mtoto, kumuua akiwa tumboni, ama kufanya mimba kutoka mapema. Hivyo unashauriwa uepuke matumizi yake.

Upo!


No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.